Karibu katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa South Nyanza Conference. Upendo wa Mungu wetu usio na kipimo na rehema zake zilizo nyingi zimetuwezesha kufika hapa. Tunapokutana kupanga mambo mbalimbali, kupokea taarifa za kazi kwa kipindi cha 2022 – 2025, hebu neno kuu la Mkutano lisemalo “Yesu Anakuja, Nitakwenda” litukumbushe wito wetu mkuu na muhimu wa nyakati hizi.
Pr. Beatus G. Mlozi, Mwenyekiti (South Nyanza Conference 2022 – 2025)
Mkutano Mkuu ni zaidi ya kusanyiko la kuchagua watendakazi tu, ni udhihirisho wa kipekee wa namna Mungu anavyoliongoza Kanisa lake katika nyakati hizi za kufunga historia ya ulimwengu. Ni mahali wanapokutana wawakilishi kutoka maeneo yote ya Conference yetu kumshukuru Bwana, kupokea taarifa za utendaji kazi kwa muhula mzima na kuweka mipango ya namna kazi ya Mungu itafanyika kwa miaka mingine mitano.